HATUA ZA KUMFANYA MWANAMKE AMUACHE MPENZI WAKE AJE KWAKO
Kukatiza stori fupi, hapa utakuwa umebakishwa na uchaguzi miwili ambayo unapaswa kuchagua ikifikia hapa: unaweza kuamua kuachana naye, ama unaweza kuchukua hatua ya usoni. Sasa hii haimaanishi ya kwamba unapaswa huuvunja uhusiano ambao tayari yuko nao ama tayari anafurahia. Lakini, kama anaonekana kuwa hajapendezwa na mahusiano ambayo tayari yuko, ama umeingiwa na hamaki ya kumtaka awe girlfriend wako, basi kuna hatua kadhaa ambazo unaweza kuzitumia ili umfanye aachane na mpenzi wake na akufuate wewe.
Hatua #1 Chambua mahusiano yako
Kabla kuchukua hatua yeyote lazima uchambue mahusiano yake na wewe. Je anakuchukuliaje? Kama amekuingiza katika himaya ya urafiki, basi tatizo hapa halitakuwa kwa boyfriend wake bali uhusiano wake na wewe wa kirafiki. Wanawake huwa na fikra mbilimbili kabla hawajaanza kudeti marafiki zao wa dhati kwa kuwa hawataki kuharibu uhusiano wao wa kirafiki nao.
Katika kesi nyingine, wanawake wanakuwa marafiki wazuri na mwanaume kiasi cha kuwa hawaingiwi na mawazo ya kuwa wanaweza kuwadeti hata kama wako single. Hii inaweza kuwa kama kesi unayoipitia sahizi. Hili neno ‘friend zone’/himaya ya urafiki linatumika sana na wanaume wengi wanafanya makosa mpaka wanajikuta wameingizwa katika shimo hili ambalo ni vigumu kujinasua – hili jambo liko na linakera sana. Kama umenaswa katika hili jinamizi na ‘friend zone’ na mwanamke unayempenda, basi fanya hima hima ujinasue na ufuate mbinu thabiti ambazo zitakujeuza mwanaume tofauti ambaye anaweza kudeti naye.
Hatua #2 Jifanye kama uko single
Baada ya kuchambua mahusiano yenu, anza kufikiria mambo ambayo munaweza kuyafanya mkiwa pamoja na mambo ambayo hupaswi kufanya akiwa na wewe. Mfano hupaswi kuleta stori za kumhusu mpenzi wake, ili uweze kumsoma kiwango gani ambacho anacho ikija kwa kumpenda mpenzi wake.
Kama hamzungumzii kuhusu mpenzi wake mara kwa mara katika maongezi yenu, basi itakuwa ni ishara ya kwanza kuonyesha kuwa hayuko interested na yeye sana. Hii itakurahisishia kazi kwako kuweza kumnasa kiurahisi. Kile ambacho unahitaji kufanya nikumsuka zaidi, ongea na yeye vile ambavyo anataka uongee naye, na pia mfanye akuone kuwa unavutia kadri wakati unavyosonga.
Hatua #3 Linganisha ustadi wako wa mahusiano
Wakati huu, nni wakati wa kujilinganisha wewe na boyfriend wake kinjia fioa, yaani kujipima uwezo wako na boyfriend wake kichinichini. Kwa kuanza mambo, unapaswa kuongea kuhusu vile ambavyo unaweza kuwa boyfriend mbaya kwa sababu unapenda maisha sana. Mbinu hii ya maongezi ni ya viini macho ambayo tuliieleza kwa kina awali katika machapisho yenu. Huku kutamfanya mwanamke kutaka kujua ni kwa nini unapenda maisha, na ni kivipi utakuwa boyfriend mbaya kwake. Pia katika mazungumzo yako, muelezee ni kivipi unayapenda maisha yako na jinsi unavyoishi. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke ajenge picha ya maisha yako akiwa na wewe. Utamsisimua na kumfanya akuone kuwa maisha yako ni ya furaha wakati wote.
Kwa kufuata hatua muhimu, unaweza kuiba atenshen ya mwanamke ije kwako, na kuweza kumuwini mwishowe hata kama tayari ana boyfriend – aminia hili. Pindi utakapofanikiwa, anaweza kukuonyesha hata dalili za kuwa ameanza kufall na wewe na kumuacha mwanaume aliyempenda awali kabisa...
Upo!
No comments