kotii

kotii

JE, UNAJUA UMUHIMU WA BODY SCRUB NA JINSI YA KUICHAGUA YA KUKUFAA WEWE?

JE, UNAJUA UMUHIMU WA BODY SCRUB NA JINSI YA KUICHAGUA YA KUKUFAA WEWE?


Wapenzi hali zenu?
Natumaini kwa wema wa MUNGU unayesoma hapa u mzima na kama mambo yako hayasomeki basi nikupe moyo, utapita tu huo wakati mgumu.
Tuzungumzie body scrub, wengi tunaisikia tu labda na wengine labda tukienda kwa wapaka rangi wenye mbwembwe wanatuscrub tu na chochote kinachoitwa scrub.



UMUHIMU WA BODY SCRUB

Kinachotofautisha body scrub na visafisha ngozi vingine( cleansers) kama cleanser,bath gell na body wash ni kwamba scrub ina chembe chembe (texture) zinazoiwezesha kufanya kazi katika kuisugua ngozi ya mtumiaji. 
 
Kazi zinazofanywa na body scrub ni kama ifuatavyo:-
  • Kuondoa seli zilizokufa, hizi hutengeneza kama layer flani ya uchafu juu ya ngozi.
  • Inasaidia kuiacha ngozi yako ikiwa ya kung'aa na muonekano mzuri.
  • Inaondoa mafuta na vipodozi vinavyoziba matundu ya ngozi yako.
  • Inapunguza na kuzuia kuota chunusi.
  • Inasaidia ngozi yako kuweza kufyonza vizuri mafuta/lotion na virutubisho vingine vya kupakwa.

UTACHAGUAJE YA KUKUFAA?

Vitu vinavyoamua uchague scrub ipi ni vifuatavyo: 

AINA YA NGOZI YAKO: 

Aina ya chembe chembe katika scrub yako ichaguliwe ukijua ngozi yako ya namna gani.

Ngozi Kavu 
Iwapo una ngozi kavu basi chagua scrub zenye mafuta yanayoweza kulainisha ngozi mfano ukiona moja ya viungo ni almond oil, butter au milk itakufaa, ikiwa na chocolate, brown sugar na coffee kama chembe chembe zilizoungwa basi ngozi yako kavu imefika.

Ngozi yenye mafuta mengi 
Iwapo una ngozi yenye mafuta mengi, chagua scrub isiyo na mafuta. Viungo muhimu katika scrub ya mtu mwenye ngozi ya mafuta ni papaya, lemon(limao), Apricot na oatmeal kwa hiyo bidhaa yenye kati ya hivyo ni yako mwenye ngozi ya mafuta.


Ngozi inayopata mabadiliko ghafla( sensitive skin) na kavu sana.
Iwapo una ngozi ya namna hii ni vema ukachagua scrub yenye chembe chembe ndogo ndogo kama scub ya sukari, cha muhimu hakikisha unasafisha vizuri zinapodondoka usialike sisimizi. mtu mwenye ngozi hii asitumie chumvi kama scrub.


HARUFU YA SCRUB

Unapochagua scrub angalia harufu unayoipenda, inayokufanya ujisikie vizuri ambayo si kali iwapo wewe una allergy isikusumbue. Jambo jingine harufu nzuri ya scrub inaweza kuwa kama matibabu ya kukufanya ujisikie amani na utulivu ( Aroma Therapy) kwa hiyo harufu inaweza kuwa moja ya vigezo muhimu.


VIUNGO VYA KEMIKALI

Baadhi ya scrub zina viungo asilia vya kurutubisha ngozi na zingine huwa na kemikali, angalia hili pia. Glycolic au salicylic acid ni baadhi ya viungo hivyo (active ingridients) vinavyoongeza nguvu ya scrub katika kufanya kazi kwake. Baadhi zikiwa na viungo hivi hufaa kwa watu wenye kupata chunusi mara kwa mara hivyo hupunguza au kuondoa kabisa tatizo na pia kwa ngozi inayozeeka kwa watu wenye umri mkubwa.


BEI (BUDGET)

Angalia uwezo wako wa kumudu gharama maana sio lazima ununue scrub ya gharama maana saa zingine viungo ni vile vile tu, tazama viungo kisha angalia bei.

JINSI YA KUTUMIA SCRUB

Jitahidi usitumie nguvu nyingi katika kusugua ngozi yako maana unaweza kujichubua na chembe chembe za scrub yako.

Sugua ngozi yako kwa kufuata uelekeo wa viduara kuifanya isugue vizuri.

Scrub zenye mafuta unaweza kutumia kwenye ngozi kavu au ikiwa na maji ila inashauriwa kwa watu wenye ngozi kavu wajiloweshe na maji kwanza ndio wa-scrub ngozi zao kwa hiyo mtu anaweza kuoga kwanza au kunawa uso kabla ya kuanza kuitumia.


Unaweza kutumia nguvu zaidi kwenye ngozi ngumu kama magotini na kwenye maungio ambapo huwa na ngozi ngumu.

Hayo kwa leo,

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();