kotii

kotii

Mambo Wanawake Hufanya Ambayo Huchukiza Wanaume

Mambo Wanawake Hufanya Ambayo Huchukiza Wanaume

Ok najua haiwezekani kukusanya wanawake wote pamoja kwa kuwa kila mwanamke ana tabia tofauti kabisa na mwengine. Na pia si wanaume wote wanaudhiwa na kitu kimoja. Lakini kwa kawaida wanaume wakati mwingine huweza kuwa na tabia za ujumla, yaani kuna mambo ambayo wanaume wa kawaida huwa nayo kwa pamoja. Hivyo tumeamua kuja na baadhi ya mambo kwa ujumla ambayo huwaudhi wanaume kutoka kwa wanawake.

Hivyo kama mwanamke unapenda baadhi ya tabia hizi basi fahamu ya kuwa unamchukiza mpenzi wako.

Kuwa na hisia nyingi
Wanaume wanaweza kupandwa na mori iwapo wapenzi wao wanakuwa na hisia za kupindukia, sana sana kama wanaanza kulia halafu wanatarajia wanaume kutatua matatizo yao. Wanaume hujua ya kuwa wanawake huwa na hisia nyingi kuanzia kufunja kucha zao ama kusongwa nywele vinaya, wanaume wengi hukiri ya kuwa ni vigumu kwao kuweza kutatua baadhi ya matatizo yao.

Kuwa mzuri kuliko mwengine
Wanawake wanapenda sana kuwasifia wapenzi wao kuwa ni wazuri na eti ni tofauti kuliko wapenzi wake wa zamani. Mara ya kwanza kwanza mwanamume atapenda kusikia maneno kama hayo na kuona kama ulipitia pabaya wakati wa mahusiano yako na wengine lakini baada ya muda ataanza kufikiria kuwa wewe utamwingiza katika moja wapo la kundi ambalo atakuwa ukimuita 'mwanamume fala'. Njia nzuri ya kutatua jambo hili ni kusema ya kuwa hjawahi kuwa katika mahusiano yeyote na mwanamume hivyo mtakuwa na wakati mzuri pamoja. 
Kuongea bila kikomo
Wanawake wanapenda sana kuongea kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi na marafiki zao wanawake. Lakini hio ni tofauti  kwani wanaume hawapendi sana kuzungumza mengi so kama una maneno mengi yasiyokuwa na mwisho basi itakubidi uachane na hio tabia.

Shopping isioisha
Ukweli usemwe ni kuwa wanawake hupenda sana kufanya shopping kiasi cha kuwa inafikia wakati fulani kunaboa. Sasa kama wewe ni mwanamke unayependa kufanya shopping usijaribu kuenda shopping na mpenzi wako. Tabia ya kuingia kwa duka kwa masaa mawili kununua dress na mpenzi wako kutakutia taabani. Hii ni kwa sababu ya kuwa muda mwingi mwanamume hatakuwa na kitu cha kufanya ila kukuangalia tu wewe. Pia tabia ya kufalia nguo halafu kumuuliza kama nguo iliyofaa inakupendeza au la ni kuchosha kwake.


Kama unamambo mengine ambayo huchukiza wanaume kutoka kwa wanawake unaweza kuweka comment yako hapo chini

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();