Kamati ya katiba, sheria kujadili kesi 13 pamoja na ya mchezaji Hassan Kessy
Kamati ya katiba, sheria kujadili kesi 13 pamoja na ya mchezaji Hassan Kessy
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji leo Jumamosi Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13.
Malalamiko hayo ni:
1.Mchezaji Ametre Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa pamoja na kufikia mafaka.
2. Klabu ya Coastal Union dhidi ya Simba kuhusu madai ya fidia kwa wachezaji Hamad Juma na Abdi Banda.
3. Ally Rashid Ally dhidi ya Simba, malalamiko ya kunyimwa stahiki zake
4. Mchezaji Abdallah Juma dhidi ya Mbeya City, madai ya malimbikizo ya mshahara, fedha za usajili na gharama za matibabu.
5. Simba dhidi ya Young Africans, madai ni kuingia mkataba na mchezaji Hassan Kessy wakati ana mkataba na Klabu ya Simba
6. Kocha Abdul H. Banyai, kesi ni madai ya stahiki zake.
7. Coastal dhidi ya Young Africans, madai ya fidia ya matunzo ya mchezaji Juma Mahadhi
8. Saleh Malande dhidi ya Ndanda FC madai ya uvunjikaji wa mkataba
9. Coastal Union dhidi ya Mbeya City, madai ya fidia ya fidia kwa matunzo ya mchaji wao.
10. Sputanza FC dhidi ya Mbeya City, madai ya ada na usajili na mishahara
11. Kimondo FC dhidi ya Ruvu JKT, majibu ya kumalizana kati ya timu hizo mbili
12. Mathias Lule dhidi ya Stand United, taarifa ya kushindwa kufikia makubaliano ya kulipana.
13. Kimara United FC dhidi ya Kurugenzi FC, pingamizi la mchezaji Martine Sepeni kusajili timu ya Kurugenzi ya Iringa.
No comments