kotii

kotii

Khalfan akanusha bifu na Hanscana



Muongozaji wa video hapa nchini Tanzania, Director Khalfan adaiwa kutokuwa karibu tena na muongozaji mwenzake, Hanscana, kisa kikidaiwa kuwa ni Wanene Entertainment ambapo hapo awali walikuwa wakifanya baadhi ya kazi kwa pamoja.


Director Khalfan (kushoto) na Hanscana
Siku za nyuma habari zilivuma juu ya kuondoka kwa Hancana kwenye kampuni hiyo ya Wanene Entertainment lakini Khalfan kwake imekuwa ni kama kuokota dhahabu mchangani.
eNewz iliamua kujiridhisha kutaka kujua kama kweli wamegombana kwa sababu ya mtonyo huo ambapo Khalfan alikanusha na kusema yeye na Hanscana wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja hivyo sio rahisi kwa wao wakatemana.
“Hanscana ni mwanangu wa damu, siwezi kutofautiana naye kwa kitu kidogo. Hanscana ametoka Wanene kwa maslahi yake mwenyewe lakini amekuwa akinishauri ni nini nifanye nikiwa Wanene ili nifanye vizuri, Hauwezi ukatofautiana na kaka yako” Alisema Khalfan.
Lakini pia Khalfan amesema kuwa maneno ya wao kugombana yanazalishwa na mashabiki mtaani kwa kuzipambanisha kazi zao pasipo kujua kuwa wao wanafanya kazi kwa pamoja.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();