kotii

kotii

Nuh Mziwanda amkacha Petit man


Meneja wa wasanii hapa nchini, Petit man anazidi kukimbiwa na ambao amekuwa akiwasimamia ikiwa ni kuanzia kwa Wema Sepetu, Miror na sasa ni Nuh Mziwanda.
Petit man akiwa na Nuh Mziwanda.
Kupitia eNewz ya EATV, mwanamuziki wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kuacha kufanya kazi akiwa chini ya Petit ili kuhakikisha muziki wake unakuwa tofauti na alivyo sasa.
Mziwanda amesema “Mimi ni msanii mkubwa, Inabidi kuwe na tofauti kati ya nikiwa na menejiment na wakati sina menejiment, Petit amenikuta nikiwa na jina tayari nimesha'hustle' hadi akanikuta nina jina. Niliona nifanye naye kazi kwakuwa ni kijana mwenzangu”
Nuh Mziwanda alizidi kufunguka kuwa kwenye miaka mitatu ameona hamna utofauti katika muziki wake mbali na alivyo kuwa yeye pekee bila kusimamiwa naye “Lazima ajue kuwa kama meneja ni vitu gani avifanye ili msanii akue, Kunavitu ambavyo amekuwa akishindwa kuvipendekeza kwangu ili nikue”
Nuh amefunguka kuwa kwa miaka mitatu ameona anashuka kimuziki kitu ambacho hakitaki na hayupo tayari kuona anashuka kimuziki hata kama mpenzi wake atakuwa na mchango katika hilo.
Lakini pia Mziwanda ameweka wazi kuwa hana tofauti na Petit na hata ikitokea kazi ya kufanya naye atakuwa tayari kwa kuwa wote wanatafuta pesa.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();