TIA YOTE. SEHEMU YA 23
SIMULIZI...TIA YOTE
SEHEMU YA 23
NA:GAO
CALL:0654387935
ILIPOISHIAAA.....katika juhudi za kurudi nyumbani baada ya kutoka kwa mama imma, nilitembea na giza ndipo watu nisio wafahamu tena hata sauti zao zilikuwa ngeni masikioni mwangu sikuweza kujitambua, hapo walinizunguka huku mikononi na silaha zao walipo nizunguka huku wakibisha bishana hapi mmoja wao akanifata pale katikati...........
ENDELEAAAAAAAAAAA.................. Nilihisi marue rue..
"Wewe nani na unatoka,?"ni swali la kwanza aliloniuliza, yule alienifata pale katikati.
Nikikosa cha kumjibu kwa woga ulionikaa usiku ule.
"Bhan oya anachereweshwa nini huyo apigwe tu, mwizi"alisema mmoja wao mkono kashikilia panga, nililoliona kupitia mwanga wa torch.
"Tulia, kwanza wewe."
"Aahh, tulia nini huyo apigwe au tumpeleke kituoni akaeleze."alizidi kuchochea yule mwengine, hapo sasa kinywa changu kilikuwa tayari kufunguka.
"Jamani mimi sio mwizi,"maneno yalinitoka.
"Sio mwizi unatoka wapi peku peku hivyo."nilikuwa sijajiangalia na hata habari sina kuangalia hapo kweli viatu sina, sikuweza kuwa na kumbu kumbu sahihi juu ya nilipotupa viatu vyangu.
"Huyu ni wale wale embu nipishe"alikipenyeza mmoja aliekuwa kashika gongo, alizuliwa ila tayari alirusha gongo likanipiga la kiuno.
"Oooooh,aaaaaah"nilitoa ukelele wa maumivu.
"Bhana niacheni,sasa kazi gani ya kiboya hii mwizi huyo tumsurubu mwaleta ujinga"alisema kwa jazba.
"Jaman mimi sio mwizi nimekimbizwa kule wakati natoka nje kukojoa ndio wakatokea watu wenye mapanga na kuanza kunifukuza."nilitamka uongo uliofanana na ukweli kabisa,sikujua kama watanielewa wakati huo kiuno kinaleta shida nayasikia maumivu niliyoishia kuyavumilia tu.
Walizozana zozana, muda huo niligundua ni sungusungu,walinielewa kishingo upande upande ila yule mmoja wao hakuweza kuamini aliwalaumu sana wenzake na kutukana matusi kadhaa hasa upumbavu,ujinga na uboya, aliyatamka maneno yale kuwaambia wenzake baada ya kuniachia mimi.
"Sawa kwenu wapi.?"
"sipajui nilikimbia tu giza hili siwezi kufahamu"
"Umetokea wapi?"alizidi kuniuliza maswali ambayo sikuonesha ushirikiano, alikosa hata cha kuendelea kuniuliza hivyo alichofanya ni kuniekekeza njia ya kutokea kwenye kituo cha magari.
Nilimshukuru, kisha nikaachana nao hapo moja kwa moja nikaanza kuongoza kuifata barabara ile, njiani nilianza kujitisha mwenyewe na kuogopa kabisa, niliendelea kutembea na mwendo huo wa kuogopa ogopa.
Wakati nikitembea mwendo wa kulazimisha kiuno kishirikiane na miguu ili nwendo uendeleaa, nilishaangaa gari kubwa la mizigo likipita huku gurudumu zake ziligongana gongana kibaya zaidi halikuwa na taa, Lilitembea na giza lake bila kujali mashimo ba mabonde yaliyopo njiani hapo sasa nilibaki mdomo wazi liliponikaribia gari lile ambalo sidhani kama waliomo ndani waliniona nililiita ni gari kutokana na ukubwa wale ila lilinishangaza liliponifikia halikuwa gari kama nilivyotegemea.
Nilishaangaa sana hadi kukikuta nakimbilia mti uliokopembezoni mwa pale, hapo nilisitiri mwili wangu kutokana na woga ulionijaa,
Niliogopa sana lile halikuwa gari ila ni treni.
Sijasumbua kichwa kujua ni aina gani ya tren inayopita kwenye barabare ambayo sio yake.
Kwa woga niliishia kujibanza kwenye mti nikisubiria lipoteee katika ngoma za masikio yangu, sikuwa nikiliona zaidi ya ya mgongano wa gurudumu.
Sikuwa na habari kumbe muda unazidi kusogea tu, nilitoka mafichoni pale na kuanza kuifata njia ile, mwendo niliotembea ni kama roboti kiuno hakikuwa tayari kutoa ushirikiano niliendelea kukiradhimisha tu ilimradi nifike nyumbani japo naogopa.
Baada ya umbali kadhaa nilikaribia nyumbani kabisa ndio nipo kwenye njia ndogo ya kuingia nyumbani.
Kwa mwendo ule ule,
Mara hammadi bila kuonabnilijikuta nakanyaga mkia wa mmbwa hapo ikawa kama nimemchokoza alianza kupiga kelele za kuboha nilijilazimisha na kurusha teke lililompiga akakimbia, hapo nikapata nafasi ya kufika nyumbani.
Japo nimetumia juhudi zote mpaka nafika nyumbani ila bado ilikuwa kama nimecheza tu mana geti lilisha fungwa tayari hivyo njia ya kuingia ndani hakuna.
Kwa akili za haraka zisizotaka umakini wa kufikiri niliona nipande juu hata nilale uwani,nilisahau kama kiuno changu hakipo imala nilikifanya kuruka juu mzima mzima, kuruka niliruka vizuri kilichonikwamisha ni pale kuvuta mguu kuweka pale juu hapo niliamsha maumivu nikajikuta naanguka chini kabisa.
"Aiiiiiiiii"kelele hazikuacha nitoka, mithili ya mtu alievamia miba tena migunga, lazima kelele zikutoke.
Nilipoteza umaridadi wa kuamka pale chini, niliamua kupageuza kitanda na kulala nikijifunika ngumi.
Usiku ulikuwa mrefu sana, nikiwa nimelala sijui kinachoendelea.
Kilipita kimya hadi kujakukohoa,hiyo ndio ikawa sababu yangu ya kuamka niliamka nikifikicha macho, uchovu wa kuamka.
"Haaah nipo wapi hapa"nilijipa swali na kuamka kusimama nikishangaa shangaa, na kuondoka eneo lile kusubiri mlango ufunguliwe nipate nafasi ya kuingia ndani.
Muda mchache nilisikia ukifunguliwa, macho yote nikayaelekeza getini kuangalia anetoka,
Nilikodoa macho bila mafanikio kwani hakuna alietoka ilinibidi niende kwa tahadhali kwanza nilichungulia uwani hakuna mtu ndipo nikanyata hadi kujituliza kwenye mauwa.
nilijiona mjanja sana kumshinda sungura kumbe nipo mtegoni bila kujua.
Nilijitoa na kuufata mlango haraka haraka nikijua bado wamelala.
Ile kufinya kitasa na kuingia ndani kabla sijageuka mana nilipoufinya niliingia taratibu sikuangalia mbele nilimrudisha mlango taratibu sasa ile kuugeuka tu, shangazi huyo kasimama mbele.............................
ITAENDELEAAAAA
No comments