kotii

kotii

Baba achinja wanawe wawili kisha ajinyonga

Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo. Mawasiliano yetu 0654387935
Watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu na sita wa Kijiji cha Patane Kata ya Mambamiamba wilayani Same, wameuawa kwa kuchinjwa na panga na baba yao mzazi Yohana Greson (26) na yeye mwenyewe kujining’iniza kwenye paa la nyumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa,alitoa taarifa hizo jana kwa vyombo vya habari alisema tukio hilo lilitokea Desemba 13 saa 5 asubuhi, mwaka huu katika Kijiji cha Patane.
Kamanda alisema baba huyo alifanya tukio hilo la kutisha baada ya mkewe Eva Tumaini (29) mkazi Kijiji cha Ghona kwenda shambani na kumwacha mumewe nyumbani akiwa na watoto wawili, Esta Yohana na Tumaini Yohana, ambapo alichukua panga na kuwachinja na yeye kujinyonga kwa kamba.
Aidha kamanda Mutafungwa alisema kuwa chanzo cha mwanaume huyo kufanya mauaji hayo hakijajulikana na tukio hilo linaendelea kuchunguzwa. Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();