CDA yaonya uuzaji viwanja vilivyopimwa
Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo.
Mawasiliano yetu 0654387935
MAMLAKA ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imepiga marufuku tabia ya baadhi ya wananchi mjini Dodoma waliopimiwa viwanja vyao kihalali, kuuza maeneo yao na kwenda kuvamia maeneo mengine.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Meneja Uhusiano wa mamlaka hiyo, Angela Msimbila.
Alisema imezuka tabia isiyo sahihi ya wananchi kuvamia maeneo mengine baada ya kuuza maeneo yao yaliyopimwa na hivyo kuvuruga mpango miji.
Pamoja na kuvuruga mpango miji pia imeelezwa wanaleta adha kubwa kwa CDA pamoja na kuliingizia gharama taifa kwa kuwalipa fidia kila wanapovamia maeneo.
Alisema wakati serikali inazidi kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma, tabia za wakazi hao kuuza maeneo yao na kuvamia maeneo mengine inaleta shida kubwa. Pamoja na serikali kuanza kuhamia Dodoma kwa kuanzia na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya wizara, kumekuwepo na changamoto kubwa ya ardhi na uvamizi wa viwanja kiholela.
Msimbila anasema maeneo mengi yaliyokuwa yamepangwa kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo, mfano Nbathi, tayari yameshavamiwa. Hata hivyo, katika mahojiano na gazeti hili wananchi kadhaa walisema ugumu wa maisha unawafanya wauze viwanja vyao na kwenda kuvamia maeneo ambayo hayajapimwa.
Kumekuwepo na mahitaji makubwa ya viwanja katika maeneo yaliyopimwa hivyo kufanya biashara ya viwanja kuwa moja ya shughuli za kujikimu miongoni mwa wenyeji ndani ya manispaa.
Wakazi watatu wa manispaa ambao walizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, Daud Mtabalizo, Pelis Mwaluko na Majojo Julius wamesema zipo sababu zinazowafanya kuuza maeneo hayo ili waweze kupata fedha za kujenga nyumba za kisasa.
Walisema wanajua hawatakiwi kuuza na kuvamia maeneo mengine, lakini wanafanya hivyo ili kujipatia makazi. Agosti 25 mwaka huu, CDA ilisema imekamilisha upimaji wa viwanja 20,000 kwa ajili ya makazi na maeneo ya vitega uchumi.
Dodoma ilitangazwa kuwa makao makuu ya nchi mwaka 1973 na licha ya juhudi za serikali za kuhamia Dodoma kwa kuweka miundombinu mbalimbali kwa awamu, serikali ya awamu ya tano imeonekana kupania kutimiza dhamira hiyo, ikisema itahakikisha inahamia Dodoma kabla ya awamu yake haijamaliza mwaka 2020.
Tangu kuanza kwa harakati hizo huku Waziri Mkuu akitangulia kuhamia Dodoma, mamlaka mbalimbali zimekuwa zikitoa miongozo kuhusiana na upangaji wa mji ili uwe wa kisasa zaidi tofauti na miji mingine mikubwa kama Dar es Salaam ambayo licha ya hadhi yake, kwa kiasi kikubwa imejengwa kiholela.
Aidha, Septemba mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisitisha utwaaji wa maeneo ya wananchi unaofanywa na CDA na kuitaka mamlaka hiyo kuja na mkakati ili uweze kutangazwa kwa wananchi.
Aliitaka CDA isitishe kutwaa maeneo ya watu kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi hali ambao inaleta sura kuwa ujio wa serikali makao makuu utaathiri maisha ya wenyeji.
Aidha, Oktoba mwaka huu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliwataka watendaji CDA kubadilika ili kutofanyakazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanasimamia ujenzi unaokwenda sambamba na mipango miji.
Alisema ni wakati wa CDA kujipanga vizuri kwani kuwa Jiji sio kazi ndogo hakuhitaji kufanya kazi kwa mazoea.
“Mnafurahi serikali kuja Dodoma, lakini maumivu lazima yatakuja kuna kubomolewa pia,” alisema.
Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama alisema kazi ya kuratibu jukumu la kuhamia Dodoma inakwenda vizuri na kusisitiza hakuna shaka yoyote juu ya dhamira ya serikali yote kuhamia Dodoma kufikia mwaka 2020.

No comments