Goli la Samatta lililoiokoa KRC Genk na kipigo dhidi ya Standard Liege Dec 18 2016
Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo.
Mawasiliano yetu 0654387935
Jumapili ya December 18 2016 KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta iliwakaribisha Standard de Liege katika uwanja wao wa Luminus kucheza mchezo wao wa 18 wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017.
Genk wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walianza kupata goli la uongozi dakika ya 3 kupitia Omar Colley kabla ya dakika ya 16 Orlando Carlos kufunga goli la kusawazisha na dakika ya 25 Ishak Belfodil kuongeza goli la pili na kuanza kuwa makini na ulinzi wa goli lao kuwadhibiti Genk.
Mchezo ulienda mapumziko KRC Genk wakiwa nyuma kwa goli 2-1 hali ambayo iliwawia vigumu kupata goli la kusawazisha mapema, Samatta ndio alikuwa mkombozi wa KRC Genk baada ya dakika ya 77 kupachika goli la kusawazisha kwa kichwa kupitia krosi iliyopigwa na Jere Uronen na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2

No comments