kotii

kotii

HUYU HAPA BINADAMU WA KWANZA KUZALIWA NA KUUA

Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo.


 

[​IMG] 
Ukiachana na wanasayansi wanaotudanganya kila kukicha juu ya chimbuko la binadamu neno la Mungu linatueleza kwa kinagaubaga chimbuko la binadamu pamoja na viumbe hai wengine namna walivyoumbwa na mwenyezi Mungu kwa hiyo viumbe hai vyote na visivyo hai vimeumbwa na mwenyezi Mungu. 

Hebu leo basi tuangalie juu ya binadamu wa kwanza kabisa kuzaliwa na kuua. kadiri ya kitabu cha mwanzo (Bibilia) katika agano la kale baada ya Adam na mkewe Hawa kula tunda la kati walilokatazwa na Mungu, Mungu aliwatoa katika bustani ya Eden na kuwaamuru wakazae ili waijaze dunia.

Katika kitabu cha mwanzo kinaeleza baada ya Adam na Hawa kufukuzwa kwenye bustani ya Eden, Adam akamjua mkewe na wakapata mtoto wa kwanza KAINI na baadaye wakazaa mtoto mwingine kwa jina HABILI ambao hawa ndo wana wa kwanza wa Adam na Hawa na hawa Kaini na Habili walitunza imani yao kwa Mungu wakamtolea sadaka. 

Habili alitoa sadaka yake kwa Mungu katika wanyama bora wa kundi lake akiwa na hali ya unyenyekevu na imani naye Mungu akampokea. Tabia ya Kaini ilikuwa ya kiburi bila ya kumcha Mungu, kwa hiyo Mungu alimkataa (mwanzo 4:1-5, soma ebr 11:4, 1yoh 3:12). Tabia na maisha ya watoaji wa sadaka ina maana kuliko vitu wanavyovitoa, kwa hiyo Mungu alimwambia Kaini kuwa akitaka Mungu ampokee angepaswa kushinda dhambi iliyokuwa ikitaka kumwangamiza. Dhambi hiyo ilikuwa kama mnyama wa mwitu ajikunjaye na kuotea mlangoni ili aweze kumshambulia mtu akitoka nje (mwanzo 4:6-7). Kaini hakushinda dhambi yake na katika hasira na wivu alimuua nduguye Habili. 

Tendo lake la kutwaa uzima na ndugu yake ilidai kisasi kwa Mungu aliyetoa uhai ule, kwa hiyo Mungu alimfukuza Kaini aende mbali na mahali walipoishi watu wengine. Ingawa Kaini alidumu katika hali ya kutotubu Mungu katika huruma yake kubwa alimlinda asiuwawe kwa kisasi (mwanzo 4:8-16). Kwa hiyo katika maandiko matakatifu KAINI ndiye binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua baada ya kumuua nduguye HABILI. 
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();