Mzazi mwenza wa Rose Ndauka, Chiwaman afunga ndoa na mrembo huyu
Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo.
HAPA
HAPA
Mzazi mwenza wa msanii wa filamu Rose Ndauka, Maliki Bandawe aka Chiwaman amefunga ndoa kimya kimya na mrembo ambae jina lake halikupatikana mara moja.
Chiwaman ambaye ni baba wa mtoto mmoja ambaye alizaa na Rose Ndauka, waliachana na Rose Ndauka mwezi mmoja kabla ya tarehe yao ya kufunga ndoa.
Jumamosi hii, Chiwaman amepost picha akiwa na mke wake na kuandika:
Alhamdullilah#Married _Allah Barik… Nawashkuru wote mliokua pamoja nami insha allah mola atawalipa zaidi.
Chiwaman ambaye pia ni msanii wa kundi la TNG, hakuwahi kueleza sababu ya kuachana na muigizaji huyo wa filamu.