kotii

kotii

TIA YOTE 47

Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo. Mawasiliano yetu 0654387935
 TIA YOTE 47

NA GAO

CALL:0654387935

ILIPOISHIAAAA........ Neema alijitia midole kisha akaamka pale na kuondoka.
alipotoka na mimi nikatoka nilipojificha kisha moja kwa moja kutoka chooni hapo, nilitoka vuzuri hadi pale kwenye makochi sikumkuta Doreen ila nguo zangu zipo, nilizibeba mkuku mkuku mpaka kuingia chumbani  kwangu.........................
ENDELEEAAAAAAAAAAA
Niliingia nikiwa nimechoka mara dufu mwili ulikitamani kitanda muda wote  sikuwa na jinsi zaidi ya kuuridhisha mwili nilikipandia kitanda hapo bila ya dua walanini uchovu  niliokuwa nao si wa kawaida.
Nilijilaza mkupu mkupu tu. nilikija kustuka asubuhi ambayo siku hiyo ilikuwa ni ya shule nilishindwa hata kukiacha kitanda mwili umekataa kabisa kuamka kitandani hivyo niliendeleaa kulala tu na usingizi kunijia tena.
"Gaooo mwanangu gaoo"niliitwa hapo nikisikia kwa mbali kwa kukisia sauti ile ambayo ilijitambulisha ni ya shangazi hapo nikajivuta vuta mithili ya mlevi alietoka kupata chang'aa muda mchache.
Nilipoamka moja kwa moja nikaelekea mlangoni kufungua  nakutana na shangazi.
"habari za asubuhi mwanangu umeamka salama"
"ndio nimeamka salama sijui wewe anty"
"nimeamka pia kama unionavyo vipi shule leo"
"naenda shangazi nilipitiwa na usingizi"
"sawa mimi naenda kazini"
"sawa shangazi"
"sawa"maongezi yetu yaliishia hapo akaondoka na mimi nikajinyoosha nyoosha kisha nikajiandaa vizuri kwenda shule japo masaa yalikuwa yamesogea kidogo kama saa mbili na nusu na muda wa namba ni saa moja kasoro robo hivyo nilikuwa nimecherewa sana.
sikujali niliingia shule hivyo hivyo ma mweli sijakutana na mwalimu mpaka naingia hakuna.
Moja kwa moja nilielekea darasani kwangu tu nako kelele zilikuwa zinaendelea hawakuwa wametulia mana mitihani ishaisha wanasubiri tu kufunga shule ijumaa.
Nilipita moja moja mpaka eneo langu napo kaa siku zote nikiwaangalia wanafunzi wenzako wakicheka na kufurahi kwa kumaliza mitihani.
"mambo vip gao mzma wewe"Nikiwa nimekaa ilipenya sauti nyororo masikioni mwangu ambayo sikuijua kabisa pengine ni kwa sababu sijaizoea ndio mana hivyo ubongo wangu ulipata shida kuitambua ilipotoka hadi pale ilipomwachia kazi macho aweze kutambua niligeuka mzma mzma kuangalia sauti hiyo ni ya nani, ile kugeuka nilipata mshangao pale kukutana na sura ngrni kabisa ambayo sijawahi fikiri kama nitaongea nae alikiwa binti mrembo  anaeheshimika darasani kwa upole asie na rafiki wala mambo ya hovyo pia darasani alikuwa ni moja ya vichwa vinavyotuburuza kila mitihani.
"poa vip najma"nilimsarimia kwa uchangamfu, kiasi cha kuongea sauti ya bess la kiume.

"safi gao nilipenda kukaa na wewe tupige story mana nahisi sitakuona baada ya kufunga shule najua utashaa kusema hivyo keakuwa hatujawahi  kutana kabla ila nakuangalia sana kiasi cha kutamani hata siku moja nipige story na wewe ila unakuwaga busy sana alafu haupo shule mda mwingi."
"mmmmh, najma usijal nipo sasa tupigr story"
"sawa asante kwahilo"Maongezi yangu na Najma yalikuwa yakiendelea pale akizidi nipa kigugumizi nisijue kilichomleta kwangu japo kasema tupige story ila sikuchukulia manani sana hali iliyopelekea nimzoee tu  nakuanza kupiga nae story zilizodumu kwa muda wa masaa kadhaa na kukatishwa na kengere ya kwenda kunywa chai tuliagana na Najma pale akaondoka na mimi nilianza kumsaka Grace niliejiaminisha kuwa ni wangu peke yangu kumbe sivyo kizuri huliwa na wengi.
Sikumuona sehemu zote nilizomtafuta pale dalrasani mpaka nikatoka nje nilaiamua niende kule nyuma ya madarasa anagalau nikapunge upepo sikuwa na mzuka wa kunyea chai hivyo wenzangu walivyokuwa wakienda kwenye chai mimi nilielekea nyuma ya darasa kukaa sasa wakati nikienda kule nyuma nilishtukizwa na kicheko cha Grace ambacho niliweza kukijua wenyewe husema chako ni chako tu lazmaa ukijue hivyo nilikijue kicheko kil, sasa nikapata shauku ya kutaka kujua anacheka nini na yupo na nani ile kuangalia sikutaka kuamini kama Grace ndio amefanya vile niliumia sana.
Yani nikimshuhudia Grace akiwa kapakatwa na jamaa mmoja hivi wa kidato cha nne niliemtambua kwa sare yake alafu kuna jamaa wengine wamekaa pembeni.
Akilini mwangu niliona ule ni usaliti kabisa na nilimjua ni Ally yule mpenzi wake alieniambia wameachana.
Nilishindwa hata kwenda mbele zaidi, nilichoona ni kujiegemeza  kwenye ukuta tu kwenda mbele sikutaka anione kabisa.
"GRACE NI WA KUNIFANYIA HIVI KWELI HIVI KWANINI KAAMUA KURUDIANA NA ALLY WAKATI ALISEMA HAMPENDI NA ANANIPNDA MIMI HIVI KWANINI ANIFANYIE HIVII DAAAH,"nilijiongelea mwenyewe huku moyo wangu ukiwa mzito zaidi nikiona kitendo kile cha kinyama kabisa kunifanyia vile nilichokiwaza akikini mwangu nakijua mwenyewe.
"aaah,hakika sitapenda tena sipendi acha mapenzi yawe sitarehe sitadiriki kupenda, Grace wa kunifanyia hivi mimi aaah, sipendi tena sipendi"nilijiongelea kiujasiri tena kwa machozi kwa sauti ya chini watu wasije nisikia wakajua nimechizika bure.
Kusema ukweli niliumia sana na moyoni kujenga chuki zaidi nilichungulia tena kama nisie amini nilichokiona hapo ndio niliumia zaidi kuona akimchezea maziwa huku jamaa zake wakicheka tu.
Kiliniumiza kitendo hicho kikaperekea nijenge chuki zaidi kwa Grace nikaamua nirudi darasani  hata muda  wa chai ulikuwa haujaisha hivyo niliporudi darasani moja kwa moja nilienda hadi napo kaa na kuiinamia meza na kulala sikutaka kuongea na yoyote nilikuwa na machungu moyoni yasiolezeka.
Mawazo yote ni kwa Grace tu.
Nilishindwa kuvumilia kiasi cha kuyadhibiti machozi yasinitiririke yalinitoka huku nikifina fina kwa mbali kama nina mafua.
Masaa yalienda  tu watu kadhaa walionijua walinifata kuniuliza nina nini nilichowajibubsijisikii vizuri ninaumwa.

"gaoo unanini mbona umelala hapo kwenye meza."
"fyuuuu fyuuuu naumwa"niliongea kwa kufina,alikuwa ni Msichana mmoja alieniuliza mpka akaondoka, niliona uchungu kukaa hata darasani hasa nikimfikilia Grace mwanamke niliempenda toka moyoni, ama kweli wanawake ni vinyonga kazi kubadilika tu, yan sikuwa nikimwamini mwanamke yoyote tena, wa mwisho kuaminiwa na moyo wangu alikuwa ni Grace na hakuna mwengine,
Niliamua kuvaa sasa uhusika wa usaliti yani UKIWEMBE.
Niliendelea kufina fina  mpka moyo wangu  ukishirikiana na ubongo vikaniruhusu nitoke darasani sasa na yale mawazo yangu sijaangalie mbele ile kufika mlangoni tu nikajikuta nakumbana na madamu nilimtambua  kea harufu ya manukato yake yalionukia puani mwangu.........
iITAENDELEEAAAAAAA
 

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();