kotii

kotii

Y-Tony adai aliandika wimbo wake mpya akimuwaza Kajala, akiri kumpenda hadi anaumwa!

Tangaza nasi ili kukuza biashara yako, Leo.

Y-Tony amedai kuwa wakati anauandika wimbo wake mpya, Wivu Wangu, kichwani mwake alikuwa akimuwaza Kajala Masanja kwasababu ni mwanamke anayempenda sana.

kajala
Ameiambia Bongo5 kuwa muigizaji huyo ni mwanamke wa ndoto yake.
“Nilikuwa naandika wimbo huu kipindi yeye yupo katika akili yangu, alikuwepo katika moyo wangu kabisa . Sababu Kiukweli Kajala ni mwanamke ambaye amenifanya niweze kuandika hit song kama hiyo na kila mtu akaweza kuipokea,” amesema.
“Huo ndio ukweli, Wivu Wangu hadi unakamilika zilikuwepo hisia zake yeye nikijumlisha feeling zangu nimepata kitu kizuri. Kajala ni mwanamke ambaye nimetokea kumpenda katika celebrities wote,” ameongeza.
Y-Tony hajaishia hapo, ameendelea kuonesha hisia zake kwa mama huyo wa mtoto mmoja, Paula aliyezaa na P-Funk kwa kupost picha zake Instagram.


'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();