kotii

kotii

Wafanyabiashara ya ‘Unga’ Wabadili Mbinu

Wajibu wetu ni kukuhabarisha kukujuza kila kinachojiri katika nyanja zote za burudani na michezo, usikae mbali nasi tembelea kila siku kwa burudani zaidi itakayo kata kiu yako.


Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza kokeni na heroini.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela alisema jana kwamba wafanyabiashara hao husafirisha kemikali hizo kutoka Bara la Asia na wanapozifikisha nchini huzitumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.

“Hivi vibashirifu aina ya ephedrine mara nyingi vinatumika kutengenezea dawa za kifua lakini hawa wafanyabiashara haramu wanabadilisha mfumo wake. Wanachofanya wanachanganya na kemikali nyingine ambazo wanatengeneza dawa aina ya heroini na kokeni,” alisema.

Pia, alisema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha Serikali na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();