kotii

kotii

ZAMARADI na Kipindi Chake Kurudi Hewani Baada ya Kifungo cha TCRA

Wajibu wetu ni kukuhabarisha kukujuza kila kinachojiri katika nyanja zote za burudani na michezo, usikae mbali nasi tembelea kila siku kwa burudani zaidi itakayo kata kiu yako.



Kipindi cha runinga cha Take One cha Clouds TV kitarudi hewani mwezi huu baada ya hukumu yake ya kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iyotolewa Octoba mwaka 2016 kumalizika mwezi huu.


Zamaradi Mketema

Kipindi hicho kilifungiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

Mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema ametangaza ujio wa kipindi hicho huku akiwataka mashabiki wa kipindi hicho kutoa maoni juu ya mabadiliko ya kipindi hicho.

“Tukiwa tumemaliza likizo yetu tuliyopewa na TCRA, kipindi chetu kinarudi rasmi January hii 2017 namaanisha Take One mtangazaji wako nikiwa yuleyule Zamaradi H. Mketema,” aliandika Instagram Zamaradi.

Aliongeza, “Hebu niambie katika msimu wetu mpya unatamani kuona nini kwenye kipindi!!? Unatamani irudi vipi ili kuboreshwa!!? Nini kiongezwe!? Nini kipunguzwe!? Nipe maoni yako tafadhali nami nitayafanyia kazi,”

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yaliyorushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();