kotii

kotii

Baba adaiwa kumwingilia bintiye

Wajibu wetu ni kukuhabarisha kukujuza kila kinachojiri katika nyanja zote za burudani na michezo, usikae mbali nasi tembelea kila siku kwa burudani zaidi itakayo kata kiu yako.



Mkazi wa Mpigi Magoe, Ladslaus Kiwia (38), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akidaiwa kumuingilia kimwili mtoto wake wa kike (15) anayesoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Matosa.

Wakili wa Serikali Daisy Makakala alidai jana kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2015 na Septemba 2016 nyumbani kwake Mpigi Magoe.

“Inadaiwa ulimfanyia kitendo hicho binti yako wa kumzaa anayesoma kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Matosa, kitu ambacho ni kinyume na sheria za Jamhuri ya Muungano,” amedai wakili huyo.

Hakimu Mkazi Joyce Mushi, amesema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo lina dhamana, hivyo alimtaka awe na wadhamini wawili wa kuaminika wenye vitambulisho ambao watasaini bondi ya maandishi ya Sh1 milioni kila mmoja. Kesi itatajwa tena Aprili 20.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();