kotii

kotii

Ben Pol ashambuliwa kupost picha zake za utupu, Fd q atoa neno

BURUDANI KIGANJANI MWAKO. TANGAZA SASA......



Hitmaker wa Ngoma ya 'Phone' Ben Pol ashambuliwa kwa maneno makali baaada ya kupost picha iliyonyesha sehemu za staha wa za mwili wake kwenye mtandao wa picha wa Instagram.

watu wamemshambulia nyota huyo kwa kitendo hicho wengine walikiita ni kitendo cha kujidghalilisha pamoja na wanaume wengine.

Ben Pol aliachia picha hiyo jana kumradhi kwa picha hii.



Mkali wa Hip Hop Fid q ambaye ndio mshauri mkuu wa Ben Pol alipokuwa kwenye kipindi cha XXL jana alisema kuwa bado hajajua kilichompelekea  Ben Pol kutuma picha hizo mitandaoni
“Sijajua anataka kuongelea nini kwenye ile cover na mimi nasubiria kuangalia nini kitatokea, siwezi kusema ni kitu kibaya au kizuri kwa sababu sijajua nini anataka kufanya” alisema Fid Q.

Aliongeza, “Kwahiyo hata mimi sijui ana maana gani ndio maana nikasema tusubirie tuona ana kitu gani anakuja nacho ndipo tuanze kuzungumza kwamba ni ishu mbaya au nzuri,”

Pia rapa huyo amewataka wasanii kufuata maadili ya kazi zao kwa kuwa wasanii wakongwe waliweza kufanya muziki mzuri na kuwashawishi wazee kuamini muziki sio uhuni.

“Nijaribu kuwakumbusha wasanii kwamba muziki sio uhuni, tumeweza kuwashawishi wazee wetu kuamini muziki wetu sio uhuni ndiyo maana mpaka leo umeweza kufika hapa. Kwahiyo mimi ningesema wasanii wanatakiwa kufanya kazi nzuri ambazo zitaweza kuwafanya wao kufanya vizuri zaidi,”

Wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamepinga tukio hilo huku wakidai muimbaji huyo sio msanii na matukio hayo.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();