KWA NINI ALIMCHAGUA YEYE LICHA YA WANAUME WENGINE KUMTAKA?
Diana ni mke wa mtu. Alikuwa akila chakula cha jioni na rafiki zake wawili kwenye Mkahawa fulani uliopo mjini huku wakipiga story za hapa na pale. Wamekuwa marafiki pamoja kwa muda mrefu sana.
Kati ya hao rafiki zake wawili, mmoja bado hajaolewa na mwingine amejitoa kwa talaka katika ndoa iliyokua na kila aina ya manyanyaso, na sasa ni 'Single mother' akilea mwanae wa kiume...
"Aah kipindi kile tulikua na muda mzuri sana, kwanza tulikuwa bado wasichana wadogo" Diana akaongea huku akicheka kwa nguvu....
"Hahaa Diana, unakumbuka jinsi mama yako alivyokua anakukasirikia?" Yule rafiki yake aliyepo single akamuuliza Dayana huku akicheka....
Simu ya Dayana ikaita, alikuwa ni mume wake. Akachukua simu yake na kupokea. Rafiki zake walikuwa bado wakicheka kwa nguvu..
"Hi Honey..." Waridi akaongea, rafiki zake wakapunguza kicheko huku kicheko chao kikibadilika kuwa tabasamu katika nyuso zao wakati Waridi akiongea na simu...
"Ok my love. Nitakuwa hapo nyumbani baada ya kama saa moja tu. Nakupenda pia" Dayana akakata simu.
"Ni mume wangu, alikuwa akiniambia ameziona hereni zangu. Nilizipoteza wiki iliyopita..tulikuwa tukizitafuta kweli. Pia ameniambia niwasalimie wote.." Dayana akawaambia rafiki zake...
"Mmh shoga yetu, ulimpataje mume bora kabisa kama huyo? Me nakumbuka wangu alikuwa kauzu kweli, yaani asingeweza kufanya hivyo..sijui ilikuaje nikafunga ndoa na yule Buldoza..nashukuru Mungu niliondoka kwenye ile ndoa...vinginevyo mngenizika mapema shoga yenu.." Yule rafiki yake aliyetoka kwenye ndoa aliongea katika namna ya kuuliza...
"Kweli shoga, hebu tuambie ulimpataje huyo wa ubavu wako? Wanaume bora siku hizi wamekua bidhaa adimu kweli kwenye soko..." Yule rafiki yake aliye single nae akakazia swali la mwenzake...
Dayana akatabasamu na kuongea, "Yeye ndie aliyenipata, aliona kwamba mimi ni 'keeper' kila siku iendayo. Na najitahidi kila siku kubaki kuwa mwanamke ambae anaweza na anatamani kuni-keep...."
Yule rafiki yake aliye single akadakia na swali, "Nakumbuka jinsi wewe na huyu mumeo mlivyokutana, namaanisha kabla hajawa mumeo. Nakumbuka alikuja kwako wakati wanaume wengi kweli walikuwa wanakutaka, kwanini ulimchagua yeye? Nini ambacho ulikiona kwake kikakusimamia ujenge maamuzi ya kuwa nae katika maisha? Kwa sababu kama nakumbuka vizuri, kulikuwa na yule jamaa tajiri sana..anaemiliki maduka ya nguo na supermarket nae alikuwa anakutaka..anaitwa nani vile?
"Brian" akaitikia yule rafiki yake ambae ni mtalaka wa ndoa..
"Ndio, ndio Brian...na wote tulifikiri ungeolewa na Brian, lakini kwa mshangao wetu ukamchagua huyu ambae ni mume wako sasa hivi...tuambie ni nini kilichokusukuma ukaolewa na huyu?" Akaongea yule rafiki yake aliyepo single...
Dayana akanywa funda moja la juice na akaanza kuwajibu..
"Uko sahihi kabisa. Kila mwanamke atahitajiwa na wanaume wengi. Lakini katika maamuzi suala la utajiri sio kipaumbele. Kwangu mimi, nilikubali kuolewa na huyu niliyenae kwa sababu alionesha kunihitaji. Kumbuka kunatofauti kati ya 'kuhitaji' na 'kutaka'. Huyo mwanaume tajiri mnaezungumzia..ndio jina lake ni Brian, yeye alikuwa akinitaka na alikuwa ni mbinafsi mno..
...Ni kweli alikuwa na pesa, handsome, anaeenda na wakati yaani fashionable na wanawake wengi walikuwa wakimshobokea, alikuwa ni rahisi kunipa chochote nachotaka. Lakini hakuwa 'akinihitaji' alikuwa 'akinitaka'..
...Nasema sio suala la pesa kwa sababu pia kulikua na Kelvin yule mwenye duka la kubadilishia fedha. Hata Kelvin pia hakuonesha 'kunihitaji' bali alionesha 'kunitaka'..hakuniruhusu katika maisha yake, sikuwa na thamani yoyote kwake..aliweka ukuta mnene na mrefu kati yangu na yake. Alikuwa mpole pale tu anapotaka sex kutoka kwangu..hakuwa akinihitaji kabisa..
...Alichokua akifikiri yeye ni kwamba mimi ni mwanamke mzuri, mwanamke ninaevutia kwa matamanio yake ya mwili. Pia kulikuwa na huyu anaeitwa Dennis aliyekuwa akijitahidi kupritendi kuwa mtu ambae sio yeye. Pia alikuwepo huyu anaeitwa Danny...yeye alikuwa anaona njia ya kunipata mimi ni kuninunulia zawadi. Wote hao hakuna hata mmoja aliyenipenda kweli... Na hatimae my sweet husband akatokea katika maisha yangu na kunifanya nijihisi nahitajiwa...!"
Yule rafiki yake aliye single akauliza zaidi.., "Sasa shoga angu, mwanamke utajuaje kwamba mwanaume anakuhitaji na sio kukutaka?"
Dayana akagusa pete yake ya ndoa na kuizungusha vizuri kidoleni kisha akamjibu rafiki yake..
"Mwanaume 'anapokuhitaji' atakuambia. Atakuonesha udhaifu wake, hatajaribu kupretendi kuwa mtu ambae sio yeye. Atakuomba ushauri katika masuala mbalimbali, atakuwa akijitahidi kukueleza ni kwa namna gani unamfanya ajione bora kadiri siku zinavyosonga, utaona ushahidi wa namna mapenzi yenu yanavyombadilisha na kuwa bora zaidi. Atakubali kukosolewa na kuelekezwa, atakuonesha emotions zake, hatakuwa na hofu ya wewe kuona makovu yake..atakuwa na hofu ya kukupoteza..atajaribu ku-share na wewe mafanikio yake na kufeli kwake...
...Hatakuwa mgumu kuomba msamaha pale anapokuumiza au kukosea. Atajishusha pale panapotakiwa kushuka kwa sababu wewe ni mwanamke wake unaetaka kujenga maisha pamoja..
...Atakupa muda wake, atakua na kiu ya kuongea na wewe, atakuinua wewe kati ya wanawake wote anaowaona. Utakua mtu wake wa kwanza kuambiwa habari yoyote iwe mbaya ama nzuri au idea yoyote iliyopo kichwani mwake....
Mwanaume anaejiona yuko sahihi kwa kila kitu na bado anakwambia anakupenda, huyo mwanaume 'hakuhitaji' bali 'anakutaka'. Mwanaume kama huyo ni rahisi kukutumia na kukumwaga akikuacha na maumivu ya moyo...
...Mwanaume anaweza akawa na utajiri au asiwe tajiri, lakini swali, Je 'anakuhitaji'? Mapenzi sio mapenzi kama hakuna 'uhitaji'.
Yule rafiki yake mtalaka wa ndoa akatikisa kichwa kuonesha kuafikiana na maelezo ya Dayana..
Na Dayana akaendelea....
"Apatae mke amepata kitu chema, na ajipatia kibali kutoka kwa Mungu. Huu mstari katika Biblia una maana kubwa sana. Inamaanisha kwamba kuna aina fulani ya 'favour' ambayo mwanaume wangu aipate ninapoingia katika maisha yake..
...Sisi wanawake tumeumbwa kulea na kukuza katika namna iliyo bora..tunachohitaji ni kupewa hiyo nafasi ya kukuza na kulea. Tupatie ardhi, tutaikuza kuwa bustani, tupe mtoto, tutamlea awe mkubwa na pale mwanaume anapotupa upendo tunamfanya awe mwanaume bora tofauti na vile alivyokua awali...
...Tunajenga ngome isiyotikisika kama couples. Mwanamke hawezi kukuza na kulea mtu ambae hajaonesha nia ya kumhitaji. Tukiwa kama wanawake tunahitaji mwanaume ambae anatufanya tujihisi kuwa special. Pale mwanaume anaposhindwa kuonesha kumjali mwanamke wake, mwanamke hujihisi kuwa rejected na kutopendwa kabisa na kunyimwa nafasi ya kulea na kukuza...Lakini kuyaweza hayo yote wewe kwama mwanamke unatakiwa utambue kusudi lako, na uthamini utu wako kama mwanamke!
...Na wanaume ambao wako na wanawake ambao hawakuwahitaji, mara nyingi huwasaliti, huwapiga, huwatukana na kuwaharibia kabisa maisha yao..ni kwa sababu hawakuwahitaji katika maisha yao...
"Uko sahihi kabisa my dada". Yule rafiki yake mtalaka wa ndoa akaongea huku akikunja mikono yake kuonesha kuafiki...
"Mwanaume anaekuhitaji atakujali, atakuthamini, atakuheshimu, atakusikiliza, atakusifia, atakukosoa, atakulinda kwa sababu anakuhitaji katika maisha yake, anahitaji upate amani ya moyo..upo katika kila maamuzi anayoyaamua.
...Mwanaume anaekuhitaji atathamini ndoa yenu na kila muda ataku........."
Mlio wa sms katika simu ya Dayana ukasikika. Akachukua simu yake, akasoma sms na kutabasamu. Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa mumewe.....
"Dayana mbona unatabasamu ?" Yule rafiki yake aliyepo single akauliza...
"Dayana akawaonesha ujumbe kwenye simu yake aliotumiwa na mumewe, ilikuwa ni WatsApp, picha ya selfie ya mumewe na binti yake wa miaka minne. Binti yake alikuwa ameshika kipande cha karatasi kilichoandikwa "Wewe ni mama bora duniani"
BURUDANI KIGANJANI MWAKO. TANGAZA NASI SASA.....
BURUDANI KIGANJANI MWAKO. TANGAZA NASI SASA.....
No comments