Nuh Mziwanda azinguana na uongozi wake, adai viongozi wanataka umaarufu kuliko kazi
Nuh Mziwanda azinguana na uongozi wake, adai viongozi wanataka umaarufu kuliko kazi
Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amezinguana na uongozi wake ambao alikuwa anafanya nao kazi kwa madai umeshindwa kufanya kazi aliyoitaka.
Mapema mwaka huu Petit Man alimchukua msanii huyo na kuamua kumsimamia ikiwa ni wiki chache toka aachane na wasanii wa Endless Fame ya Wema Sepetu.
Nuh amedai yeye ni msanii mkubwa na meneja huyo ameshindwa kumfikisha pale ambapo alikuwa anataka kwenda.
“Nimetoka kule kwa ajili tu ya sababu zangu binafsi inabidi ni’move on, mi sio msanii mdogo inabidi niwe na meneja ambaye anajielewa na anajua msanii ambaye ninaye ni msanii ambaye yupo katika level gani, kama meneja anashindwa kujua msanii ambaye anafanya naye kazi siwezi kudeal naye, kwa sababu nilishapotezaga time katika muziki three years kwenye mapenzi, sa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye kanikuta tu nimeamua kufanya naye kazi, kwa hiyo ni bullshit mi naachana naye naendelea na mambo yangu mengine”, Nuh Mziwanda alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.
Aliongeza, “Siyo kwa ubaya kwa uzuri, niliamua kufanya naye kazi, lakini kashindwa kupresent kile kitu ambacho mi nilikihitaji, narudia tena mi ni msanii mkubwa, inabidi ajue msanii mkubwa inabidi awe na nini na nini, kuna vitu avijue kama meneja, sasa kufanya kazi na meneja ambaye na yeye anataka ustar, ni kitu ambacho hakiwezekani”, alisema Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda pia alisema anaamini jitihada zake ndizo zimemfikisha hapo alipo, na kukanusha kauli ambayo watu wengi wamesema kuwa kwa kuwa sasa ana studio, amekuwa na dharau kwa uongozi wake.
No comments