kotii

kotii

TIA YOTE 20

STORY......TIA YOTE~20

WRITTER........GAO

WHATSAPP..0654387935.


TOLEO LILILOPITAAA......
Nikaondoka wakati huo jua linakaribia kufutika  kabisa hivyobnikaanza kutembea hima hima kuwahi nyumbani, baada ya muda mwendo ulipoa nikasimama baada ya kuhisi nimeangusha hela.
Kitendo cha kusimama bila kutegemea mikono laini ilinishika kiuno ilinibidi nigeuke haraka, ile nageuka nikamshuhudia yule dada alienifuma na Ester wanaoitana shoga.......................

TEREMKAA NAYOO SASAAA......
Kwa akili za haraka haraka ambazo hazikuhitaji upembuzi, sikujua dhamira yake nini kunikuta nimesimama na kunifanyia vile.

"Mambo, vip mzma"alinisalimu kwa tabasamu lake, akiwa kaniachia

"Poa tu."nikajibu kwa mkato.

"Mbona ukolesi kiasi hicho kwanini.?"aliuliza.

"Nakimbizana  na giza lisije nikuta njiani,msna sijafua uniform za shule."

"ahaa,kwani watoka wapi."aliuliza tena baada ya swali la kwanza kumjibu ipasavyo.

"Natokea hapo mbele maskani."

"si ungefua mapema tu jamani,au ulichoka sana si ungempa Ester afue"alizidi ni chosha na maswali yake ya kipolice yani swali liko open lakini unauliza.
Nilichoka kwa muda mfupi.

"Jamani mbona unakuwa mkali."

"Amna maswali mengi."

"kwani kuna ubaya si ninajua tu jamani."

"Sawa."nikajibu kifupi kabisa.

"Ester nani yako.?"aliuliza tena hapo ndio kabisa nilimchoka kwa maswali yake yasio na mbele wala nyuma basi hata katikati hayana.

"Kwani wewe unataka nini.?"na mimi nikavaa upolice sasa nikampa swali.

"Amna napenda kujua tu."

"Ili,?"

"Nijue tu."

"Alafu ukishajua upate nini.?"

"mmmgh"aliguna hapo nikaondoka bila kuendelea kuongea mana mpaka wakati huo tayari giza lilianza kuumeza uso wa dunia na kuutawala.

"Gao unaenda wapi, yani nakuuliza unaondoka si ndio sawa dawa yako ndogo."alisema hapo nimetia pamba sikioni niliyaona ni maneno ya mkosaji tu yale.

"Ngoja dawa yako wewe ni kumwambia mama yako, mlichofanya na ester ngoja."alizidi kusema, hapo akijia shangazi ni mama yangu, pengine hiyo ni kutokana na kutomwambia uhusiano wetuimi ba ester pale alipo uliza labda anajua ester ni ndugu wa mule.
Nilimwacha akibwata maneno mengine ambayo hata sikuyasikia vizuri hiyo ni kutokana na mtamkaji kuwa mbali.
Nilitembea mwendo wa kijeshi jeshi kuwahi nyumbani zilikuwa ni kilometa kadhaa kufika nyumbani ila kwa mwendo ule wa hatua ndefu na kuimbia kimbia nilizidi kupunguza umbali hadi kufilia naiona nyumba yetu vilivyo, imewashwa taa usiku umefika.
Nilitembea mwendo mdogo dogo kwa tahadhali nisije kanyaga mbwa usiku mana yanapenda kulala hapo uwanjani karibia na kwetu.
Nilifanikiwa kipita hima hima mpaka nikaufikia mlango wetu mkuu kuibwa geti niksingia kwa kunyata nyata kama mwizi anaevizia nguo azianue na kuondoka nazo.
Hadi kufika katika dilisha la valandani pale, nilisikiliza kama baba yupo hajaondoka.
Nikalisogelea dirisha usawa wa karibu kabisa huku nikiyaamuru masikio yangu yote kuaikiliza ndani, nilisikiliza kwa muda nako olaa hakuna niliemsikia hata baba niliedhani yupo nae sikumsikia nilivuta nguvu na kuufata mlango kwa kunyata nyata ile nafungua tu uso kwa uso na shangazi.

"Haya, watoka wapi.?" nilikumbana na swali moja moja tokea kwa shangazi akishangaa muda alioniita na mpaka muda huo ndio naonekana.

"Nilikuwepo pale juu."nilijitetea

"Yani,nimetuma neema akuite na kakukuta amekuambia nakuita hukuja kwanini?"alizidi kuongea.

"Nisamehe shangazi nilijisahau sijaitikia wito baada ya kuona kimya."nilizidi kujitetea ila shangazi alikuwa kakasirika kwa muonekani wake tu, nilimtambua kakasirika yani mpaka hata sauti yake ilibadilika.
Muda huo tumesimama pale mlangoni, hakuendelea akaondoka zake nje.
Hapo mimi kiange ange sikiwa na chakufanya nilielekea chumbani kwangu kutulia mana mufa huo amani nilipoteza kwa nilivomchukiza shangazi.
Sikukaa ndani sana kukisahau nikazichukua nguo zangu na kutoka nazo nje tayari kwa kuzifua.
Japo hali ya hewa haikuwa rafiki ila nilizifua tu.

"Gao, mpenzi."sauti ya kike nyororo ya kuvutia iliniita na kunipa cheo cha upenzi.

"Gao si ninakuita baby wangu."alizidi kuongea hapo nikageuka moja kwa moja nikakutana na CAREEEN alieko kwenye tabasamu akimulikwa na taa nyeupe ndefu ya mshumaa,inayo angaza pale.
Nilishangaa sana Careen kuniita vile.

"Wewe ndo nini sasa hivyo."niliuliza kwa wasi wasi ulionijaa.

"Kwani nini mpenzi wangu si kawaida tu jamani."

"Kwanza nani mpenzi wako,?"nilimgeuzia kibao sasa.

"Jamani si wewe hapo."alisema huku akikaajuu ya kiti nilichokuwa nimekalia baada ya kusimama kuanika nguo, hapo na mimi nimesimama huku mkononi nimeshika nguo ya pili niliyokuwa namaliza kusuunza nikaanike.

"Wewee, ishia hapo hapo mimi sio mpenzi wako,"nilisema kinaga ubaga, yani nilimtolea uvivu.

"yan, gao leo unanambia hivyo mimi."alisema huku akitaka kulia.

"Jamani wewe si mtoto wa dhangazi ni ndugu yangu."

"Gao, unanambia mimi hivyo sawa."alisema na kuondoka huku akilia kwa kufika fina, hapo mimi sina hata habari nae tena ndio kwanza nikamaliza kufua na kuanika.
Baada ya kumaliza nikaelekea ndani moja kwa moja, na kukaa kwenye makochi pale nilikuwa peke yangu sikuona mtu wakati huo ule upweke ukapelekea na mimi niingie ndani, nikiwa na dhumuni la kuandaa vitu vya shule pamoja na kupitia pita kidogo madaftali yangu, nililitafuta begi mpaka kulitoa kisha nikaanza kusoma moja moja ili kupoteza muda na kuondoa upweke niliobaki nao pale, yalipita masaa kadhaa, ndipo jina langu likaanza kuitwa kama kawaida yake ni Ester sikucherewesha nilitoka haraka, nikijua fika chakula tayari mana hata tumbo lilianza kusononeka kwa njaa.
Nilitoka haraka ndani nikifata sauti ilipotokea,
Nilienda mpaka sehemu maalum ya kulia chakula.
Wenzangu walishaa kaa tayari ambao ni Neema,doreen,careen na ester shangazi hakuwepo, yani japo wote kasoro doreen, niligundua tabia zao za hovyo lakini mbele ya watu wengi wanaonekana wanaheshima hasa Careen.
Tulikuwa kwa kucheka kwa maongezi yaliokuwa, yakiendelea ila careen hakuwa na furaha, hata ulaji wake wa kimadoido doido ila sio ya yamoto band, ni madoido ya careen.

"Mnakula wanangu."shangazi aliongea baada ya kuja muda huo mkononi kashika mfuko mweusi unaonekana wazi unavitu ndani.

"Ndio."waliitikia baada ya kuilizwa hapo na yeye akajiunga na sisi.
Kusema ukweli Ester alikuwa mpishi sana, hasa kwa kuwa ametokea tanga yani alipika wali mtamu alioutia nashki ya iliki hivyo kuufanya unoge zaidi, hayo maharage ndio usiseme unaweza jing'ata ulimi kwa utamu.
Shangazi alifungua mfuko wake na kuzitoa ndizi alizogawa kwa kila mmoja wetu.
Na kuzipokea hapo shangazi ndio alimaliza utamu wa wali na ndizi zile nilitamani kisiishe ila tumbo nalo linamwisho nilipomaliza sahani ilitosha kabisa, tumbo kujaa.
Niliaga na kuingia chumbani kwangu, nikavaa taulo muda mchache nikaenda kuoga haraka na kuja kulala.

**************
Asubuhi na mapema nilidamka sikusubili usumbufu wa Ester kuniita itaa. Hivyo niliamka tu mwenyewe na kujiandaa kisha nikazinyoosha nguo na pas hadi kumakiza muda wa kwenda shule tayari.
Niliongoza heya heya mpaka kufika shule kumepoa siku hiyo ya ijumaa yani siku hiyo watu wengi huichanganya ni weekend. Hawafiki shule mahudhulio yanakuwa machache sana.
kwakuwa jana yake nilitoroka hivyo nilitembea kwa makini nikiwa sina habari wala taarifa mara nasikia nyuma mtu akiongea.
"Aaaaah, headmaster huyo yani ukiamua kutoroka  unatoroka tu."niliikunbuka sauti hiyo haraka nikazungusha shingo kumwangalia....................
ITAENDELEAAAAA......
.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();