Picha kwa juu ikionyesha namna Jokate alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese
Mwanamitindo maharufu nchini,Jokate Mwegelo amewataka watoto wa kike kujiamini,ili waweze kufikia mafanikio katika maisha hayo kwa kuweka juhudi katika elimu.
Jokate amesema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam
“nataka niwaambie watoto wa manzese sekondari,siri kubwa ya mafanikio ni kujiamini lakini usijiamini katika ujinga hivyo mnapaswa kujiamini katika vitu vya msingi ambavyo vitweza kusaidia jamii yetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema Jokate.
Kwa upande wake program meneja wa TAI, Edith James amesema kuwa umefika wakati wa wanawake kujiamini hasa kwa kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi na usafi wa mwili kwa ujumla hasa wakati wanapokuwa katika siku zao.
Amesema kuwa taasisi ya TAI imekuwa katika kampeni kwa zaidi ya shule kumi za mkoa wa Dar es Salaam,kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike waweze kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi.
No comments